Usimfanye ndugu Yako ajikwae
13 Kwa hiyo tusiendelee kuhukumiana. Badala yake mtu aamue kutoweka kamwe kikwazo au kizuizi katika njia ya ndugu mwingine. 15 Kama ndugu yako anahuzunishwa kwa sababu ya kile unachokula, basi huenendi tena katika upendo. Usiruhusu kile unachokula kiwe sababu ya kumwangamiza ndugu yako ambaye Al-Masihi alikufa kwa ajili yake. 17 Kwa maana ufalme wa Mungu si kula na kunywa, bali ni haki, amani na furaha katika Roho wa Mungu.