Haki kupitia kwa imani
21 Lakini sasa, haki ya Mungu imedhihirishwa pasipo sheria, ambayo Torati na Manabii wanaishuhudia. 22 Haki hii inayotoka kwa Mungu hupatikana kwa Isa Al-Masihi kwa wote wanaomwamini. Kwa maana hapo hakuna tofauti, 23 kwa kuwa wote wametenda dhambi na kupungukiwa na utukufu wa Mungu, 24 wanahesabiwa haki bure kwa neema yake kupitia kwa ukombozi ulio katika Al-Masihi Isa.