Naomi na Ruthu
1 Waamuzi walipotawala Israeli, kulikuwa na njaa katika nchi. Mtu mmoja kutoka nchi ya Bethlehemu ya Yuda, pamoja na mke wake na wanawe wawili, akaenda kuishi katika nchi ya Moabu.
16 Lakini Ruthu akajibu, "Usinisihi nikuache au niache kukufuata. Utakakoenda nami nitaenda, na wewe utakapoishi nitaishi. Watu wako watakuwa watu wangu, na Mungu wako atakuwa Mungu wangu. 17 Pale utakapofia nami nitafia hapo, na papo hapo nitazikwa. Mwenyezi Mungu na aniadhibu vikali, kama kitu kingine chochote kitanitenga nawe isipokuwa kifo."
20 Akawaambia, "Msiniite tena Naomi1:20 maana yake Kupendeza, Kufurahisha; niiteni Mara1:20 maana yake Chungu, kwa sababu Mwenyezi1:20 Mwenyezi hapa ina maana ya Shaddai kwa Kiebrania pia ms 21. amenitendea mambo machungu sana. 21 Mimi niliondoka hali nimejaa, lakini Mwenyezi Mungu amenirudisha mtupu. Kwa nini kuniita Naomi? Mwenyezi Mungu amenitendea mambo machungu; Mwenyezi ameniletea msiba."