Pular para o conteúdo
Publicidade

Rute 1

8 Ndipo Naomi akawaambia wale wakwe wake wawili, "Rudini, kila mmoja wenu nyumbani mwa mama yake. Mwenyezi Mungu na awatendee mema kama mlivyowatendea hao waliofariki, na mimi pia. 9 Mwenyezi Mungu na amjalie kila mmoja wenu maisha mema nyumbani mwa mume mwingine."

Kisha akawabusu, nao wakalia kwa sauti kubwa, 10 wakamwambia, "Tutarudi pamoja na wewe kwa watu wako."

11 Lakini Naomi akasema, "Rudini nyumbani, binti zangu. Kwa nini mnifuate? Je, mimi nitaweza tena kuwa na wana wengine ambao wataweza kuwaoa ninyi? 12 Rudini nyumbani, binti zangu; mimi ni mzee kiasi kwamba siwezi kumpata mume mwingine. Hata kama ningefikiria kuwa bado kuna tumaini kwangu, hata kama ningekuwa na mume usiku huu na kuwazaa wana, 13 je, mngesubiri hadi wakue? Mngebakia bila kuolewa mkiwasubiri? La, hasha, binti zangu. Nimepata uchungu kuliko ninyi, kwa sababu mkono wa Mwenyezi Mungu umekuwa kinyume nami!"

14 Kisha wakalia tena kwa sauti. Orpa akambusu mama mkwe wake, akaenda zake, lakini Ruthu akaambatana naye.

Veja também

Rute
Ver todos os capítulos de Rute