Pular para o conteúdo
Publicidade

Ruthu 3:9,10,17

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

9 Akauliza, "Wewe ni nani?"

Akajibu, "Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa."

10 Akamwambia, "Binti yangu, ubarikiwe na Mwenyezi Mungu. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.

17 Akaendelea kusema, "Amenipa shayiri vipimo sita3:17 Vipimo 6 vya shayiri ni sawa na kilo 15., akaniambia, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ "

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Eze 16:8Akasema, Ama! Ni nani wewe? Akamjibu, Ni mimi, Ruthu, mjakazi wako; uitande nguo yako juu ya mjakazi wako; kwa kuwa ndiwe wa jamaa aliye karibu. 10 Rut 2:20;1:8Akamwambia, Mwanangu, ubarikiwe na BWANA; umezidi kuonesha fadhili zako mwisho kuliko mwanzo, kwa vile usivyowafuata vijana, wawe ni maskini au matajiri.

    17 Akasema, Na vipimo hivi sita vya shayiri amenipa; maana aliniambia, Usiende kwa mkweo mikono mitupu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    9 Akauliza, "Wewe ni nani?"

    Akajibu, "Ni mimi Ruthu, mjakazi wako. Uitande nguo yako juu yangu, kwa sababu wewe ndiwe jamaa wa karibu wa kutukomboa."

    10 Akamwambia, "Binti yangu, ubarikiwe na Bwana. Wema huu wa sasa ni mkuu kushinda hata ule ulioonyesha mwanzoni. Hukuwakimbilia vijana, wakiwa matajiri au maskini.

    17 Akaendelea kusema, "Amenipa shayiri vipimo sita3:17 Vipimo sita vya shayiri ni sawa na kilo 15. akisema, ‘Usiende kwa mama mkwe wako mikono mitupu.’ "

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Rute
Ver todos os capítulos de Rute