Pular para o conteúdo
Publicidade

Tiago 4

Kujivuna kwa ajili ya kesho

13 Basi sikilizeni ninyi msemao, "Leo au kesho tutaenda katika mji huu ama ule tukae humo mwaka mmoja, tufanye biashara na kupata faida." 14 Lakini hamjui hata litakalotukia kesho. Maisha yenu ni nini? Ninyi ni ukungu ambao huonekana kwa kitambo kidogo kisha hutoweka. 15 Badala yake, inawapasa kusema, "Kama Mwenyezi Mungu akipenda, tutaishi na kufanya hili ama lile." 16 Ilivyo sasa, mnajisifu na kujigamba. Kujisifu kote kwa namna hii ni uovu. 17 Basi mtu yeyote anayejua jema limpasalo kutenda, lakini asilitende, mtu huyo anatenda dhambi.

Veja também