Pular para o conteúdo
Publicidade

Tito 1:5-9

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Sifa za wazee wa kundi la waumini

5 Sababu yangu ya kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwateua wazee wa kundi la waumini katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kundi la waumini asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waumini, wala hawashtakiwi kwa ufisadi. 7 Kwa kuwa mwangalizi wa kundi ni wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 8 Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake. 9 Lazima alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, ili aweze kuwatia moyo wengine kwa mafundisho yenye uzima na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Kwa sababu hii nilikuacha Krete, ili uyatengeneze yaliyopunguka, na kuwateua wazee katika kila mji kama vile nilivyokuamuru; 6 1 Tim 3:2-7ikiwa mtu hakushitakiwa neno, naye ni mume wa mke mmoja, ana watoto waaminio, wasioshitakiwa kuwa ni wafisadi wala wasiotii. 7 1 Kor 4:1;1 Pet 5:2;2 Tim 2:24Maana imempasa askofu1:7 Askofu: maana yake ni, Mwangalizi. awe mtu asiyeshitakiwa neno, kwa kuwa ni wakili wa Mungu; asiwe mtu wa kujipendeza nafsi yake, asiwe mwepesi wa hasira, asiwe mlevi wala mgomvi, asiwe mpenda mapato ya aibu; 8 bali awe mkarimu, mpenda wema, mwenye kiasi, mwenye haki, mtakatifu, mwenye kudhibiti nafsi yake; 9 Tit 2:1;1 Tim 1:10;2 Tim 4:3akilishika lile neno la imani vile vile kama alivyofundishwa, apate kuweza kuwaonya watu kwa mafundisho yenye uzima, na kuwashinda wenye kupinga.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Sababu ya mimi kukuacha huko Krete ni ili uweke utaratibu mambo yale yaliyosalia na kuwaweka wazee wa kanisa katika kila mji, kama nilivyokuagiza. 6 Mzee wa kanisa asiwe na lawama, awe mume wa mke mmoja, mtu ambaye watoto wake ni waaminio na wala hawashtakiwi kwa ufisadi. 7 Kwa kuwa mwangalizi, kama wakili wa Mungu, imempasa kuwa mtu asiye na lawama, asiwe mwenye majivuno au mwepesi wa hasira, wala mlevi, wala asiwe mtu mwenye tamaa ya mapato yasiyo ya halali. 8 Bali awe mkarimu, anayependa mema, mwenye kiasi, mwenye haki, mwadilifu, mnyofu, mtakatifu na mwenye kuitawala nafsi yake. 9 Inampasa alishike kwa uthabiti lile neno la imani kama lilivyofundishwa, kusudi aweze kuwaonya wengine kwa mafundisho manyofu na kuwakanusha wale wanaopingana nayo.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.

Tito
Ver todos os capítulos de Tito