Kumwombolezea yule aliyechomwa mkuki
10 "Nami nitamiminia nyumba ya Daudi na wakazi wa Yerusalemu roho ya neema12:10 au Roho wa neema na maombi. Watanitazama mimi, yule waliyemchoma. Nao watamwombolezea kama mtu anayemwombolezea mwanawe wa pekee na kusikitika kwa uchungu kama anayemsikitikia mzaliwa wake wa kwanza wa kiume.