16 Kisha walionusurika katika mataifa yote ambayo yaliushambulia Yerusalemu watakuwa wakipanda Yerusalemu kila mwaka kumwabudu Mfalme, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni na kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 17 Ikiwa taifa lolote la dunia hawataenda Yerusalemu kumwabudu Mfalme, Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, mvua haitanyesha kwao. 18 Ikiwa watu wa Misri nao hawataenda kushiriki, hawatapata mvua. Mwenyezi Mungu ataleta juu yao tauni ambayo itayapiga mataifa ambayo hayataenda kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda. 19 Hii itakuwa adhabu ya Misri na adhabu ya mataifa yote yale ambayo hayataenda Yerusalemu kuadhimisha Sikukuu ya Vibanda.
20 Katika siku hiyo, kengele zilizofungwa kwenye farasi zitaandikwa maneno haya: "Takatifu kwa Mwenyezi Mungu". Navyo vyungu vya kupikia katika nyumba ya Mwenyezi Mungu vitakuwa kama bakuli takatifu mbele ya madhabahu. 21 Kila chungu kilicho Yerusalemu na Yuda kitakuwa kitakatifu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni, na wote wanaokuja kutoa dhabihu watachukua baadhi ya vyungu hivyo na kupikia. Katika siku hiyo hatakuwepo tena mfanyabiashara katika nyumba ya Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni.