Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Wakorintho 11:20-22

SRUV Swahili Revised Union Version

20 Basi mnapokutanika pamoja haiwezekani kula chakula cha Bwana; 21 kwa maana kila mmoja hutangulia kutwaa chakula chake katika kule kula; hata huyu ana njaa, na huyu amelewa. 22 Yak 2:5,6Je! Hamna nyumba za kulia na kunywea? Au mnalidharau kanisa la Mungu, na kuwatahayarisha hao wasio na kitu? Niwaambieni? Niwasifu? La! Siwasifu kwa ajili ya hayo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    20 Mkutanikapo pamoja si Chakula cha Bwana Isa mnachokula, 21 kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa. 22 Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kundi la waumini la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu kuhusu jambo hili? La, hasha!

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    20 Mkutanikapo pamoja si chakula cha Bwana mnachokula, 21 kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa. 22 Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kanisa la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu juu ya jambo hili? La, hasha!

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.