20 Mkutanikapo pamoja si Chakula cha Bwana Isa mnachokula, 21 kwa kuwa mnapokula, kila mmoja wenu anakula bila kuwangoja wengine. Mmoja hukaa njaa na mwingine analewa. 22 Je, hamna nyumbani kwenu ambako mnaweza kula na kunywa? Au mnalidharau kundi la waumini la Mungu na kuwadhalilisha wale wasio na kitu? Niwaambie nini? Je, niwasifu kuhusu jambo hili? La, hasha!
Kushiriki Chakula cha Bwana Isa
(Mathayo 26:26-29; Marko 14:22-25; Luka 22:14-20)