1 Rum 15:25-26;Mdo 11:29;Gal 2:10;2 Kor 8:9 Kuhusu ile michango kwa ajili ya watakatifu, kama vile nilivyoamuru makanisa ya Galatia, nanyi fanyeni vivyo hivyo. 2 Mdo 20:7 Siku ya kwanza ya juma kila mmoja wenu na aweke akiba kwake, kwa kadiri ya kufanikiwa kwake; ili kwamba michango isifanyike hapo nitakapokuja; 3 nami nitakapofika nitawatuma kwa barua wale mtakaowachagua, wachukue hisani yenu mpaka Yerusalemu. 4 Na kama ikifaa niende na mimi, watasafiri pamoja nami.
5 Mdo 19:21 Lakini nitakuja kwenu, nikiisha kupita kati ya Makedonia; maana napita kati ya Makedonia. 6 Rum 15:24;Tit 3:12 Labda nitakaa kwenu; naam, labda wakati wote wa baridi, mpate kunisafirisha kokote nitakakokwenda. 7 Mdo 20:2;18:21 Maana sipendi kuonana nanyi sasa, katika kupita tu, kwa sababu natarajia kukaa kwenu muda kidogo, Bwana akinijalia. 8 Law 23:15-21;Kum 16:9-11;Mdo 19:1,10 Lakini nitakaa Efeso hadi siku ya Pentekoste; Mdo 19:8-109 2 Kor 2:12;Kol 4:3;Ufu 3:8 kwa maana nimefunguliwa mlango mkubwa wa kufaa sana, na wako wengi wanipingao.
10 1 Kor 4:17;Flp 2:20 Lakini, Timotheo akija, angalieni akae kwenu pasipo hofu; maana anaifanya kazi ya Bwana vile vile kama mimi mwenyewe; 11 1 Tim 4:12 basi mtu yeyote asimdharau, lakini msafirisheni kwa amani, ili aje kwangu; maana ninamtazamia pamoja na ndugu zetu. 12 1 Kor 1:12;3:6 Lakini kuhusu Apolo, ndugu yetu, nilimsihi sana aje kwenu pamoja na hao ndugu; ambaye si mapenzi yake kwenda sasa; lakini atakuja atakapopata nafasi.
13 Zab 31:24;Efe 6:10 Kesheni, simameni imara katika imani, iweni na ujasiri, mkawe hodari. 14 Mambo yenu yote na yatendeke katika upendo.
15 1 Kor 1:16;Rum 16:5 Tena ndugu, nawasihi; (mnawajua watu wa nyumbani mwa Stefana kwamba ni malimbuko ya Akaya, nao wamejitia katika kazi ya kuwahudumia watakatifu); 16 Flp 2:29 watiini watu kama hawa, na kila mtu afanyaye kazi pamoja nao, na kujitaabisha. 17 Nami nafurahi kwa sababu ya kuja kwao Stefana na Fortunato na Akaiko; maana hawa wamenikirimia kwa wingi yale niliyopungukiwa kwenu. 18 1 The 5:12 Maana wameniburudisha roho yangu, na roho zenu pia; basi wajueni sana watu kama hao.
19 Mdo 18:2,18,26;Rum 16:3,5 Makanisa ya Asia wawasalimu. Akila na Priska wawasalimu sana katika Bwana, pamoja na kanisa lililoko ndani ya nyumba yao. 20 Rum 16:16;2 Kor 13:12;1 Pet 5:14 Ndugu wote wawasalimu. Salimianeni kwa busu takatifu.
21 Kol 4:18;2 The 3:17 Hii ni salamu yangu Paulo kwa mkono wangu mwenyewe. 22 Gal 1:8,9 Mtu awaye yote asiyempenda Bwana, na awe amelaaniwa. Maranatha.16:22 Maranatha: maana yake ni, Bwana wetu anakuja.23 Neema ya Bwana Yesu na iwe pamoja nanyi. 24 Pendo langu na liwe pamoja nanyi nyote katika Kristo Yesu.