Publicidade

Provérbios 28

1 Waovu hukimbia wasipofuatiwa na mtu;

Bali wenye haki ni wajasiri kama simba.

2 Kwa sababu ya maasi ya nchi wakuu wake huwa wengi;

Bali kwa wenye ufahamu na maarifa hali ya nchi hudumishwa

3 Mtu mhitaji awaoneaye maskini,

Ni kama mvua ya dhoruba isiyosaza chakula.

4 Wao waiachao sheria huwasifu waovu;

Bali wao waishikao hushindana nao.

5 Watu waovu hawaelewi na haki;

Bali wamtafutao BWANA huelewa na zote.

6 Afadhali maskini aendaye katika unyofu wake,

Kuliko mpotovu wa njia angawa ni tajiri.

7 Yeye aishikaye sheria ni mwana mwenye hekima;

Bali aliye rafiki wa walafi humwaibisha babaye.

8 Yeye azidishaye mali yake kwa riba na faida,

Humkusanyia mtu awahurumiaye maskini.

9 Yeye aligeuzaye sikio lake asiisikie sheria,

Hata sala yake ni chukizo.

10 Kila mtu awapotezaye wenye haki katika njia mbaya,

Ataanguka katika rima lake mwenyewe;

Bali wakamilifu watarithi mema.

11 Mtu tajiri ana hekima machoni pake mwenyewe;

Bali maskini mwenye ufahamu humchunguza sana.

12 Wenye haki washindapo, uko utukufu mwingi;

Bali waovu waondokapo, watu hujificha.

13 Afichaye dhambi zake hatafanikiwa;

Bali yeye aziungamaye na kuziacha atapata rehema.

14 Mwanadamu mwenye kicho yu heri sikuzote;

Bali mshupavu wa moyo ataangukia madhara.

15 Kama simba angurumaye, na dubu mwenye njaa;

Ndivyo alivyo mtu mbaya awatawalaye maskini.

16 Mkuu aliyepungukiwa na akili huwaonea watu sana;

Bali achukiaye kutamani ataongeza siku zake.

17 Aliyelemewa na damu ya mtu

Atalikimbilia shimo; wala mtu asimzuie.

18 Aendaye kwa unyofu ataokolewa;

Bali mkaidi wa njia zake ataanguka mara.

19 Alimaye shamba lake atakuwa na chakula tele;

Bali afuataye mambo ya upuzi atapata umaskini wa kumtosha.

20 Mtu mwaminifu atakuwa na baraka tele;

Lakini afanyaye haraka kuwa tajiri hakosi ataadhibiwa.

21 Kupendelea watu si kwema;

Wala mtu kuasi kwa ajili ya kipande cha mkate.

22 Mwenye husuda afanya haraka kuwa tajiri;

Wala haufikiri uhitaji utakaomjia.

23 Amkemeaye mwenzake hatimaye atapata kibali;

Zaidi ya mtu ajipendekezaye kwa ulimi wake.

24 Aibaye mali ya babaye au mamaye, na kusema, Si kosa;

Mwana huyo ni rafiki wa mtu mharibifu.

25 Mwenye nafsi ya kutamani huchochea fitina;

Bali amtumainiye BWANA ataneemeshwa.

26 Mwenye kujitumainia moyo wake ni mjinga;

Bali yeye aendaye kwa busara ataokolewa.

27 Mwenye kuwagawia maskini hatahitaji kitu;

Bali afichaye macho yake atakuwa na laana nyingi.

28 Wasio haki wainukapo, wanadamu hujificha;

Bali waangamiapo, wenye haki huongezeka.

Veja também

Publicidade
Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-06-16_06-50-08-