8 Lakini nawaambia wale wasiooa bado, na wajane, Ni heri wakae kama mimi nilivyo. 9 1 Tim 5:14Lakini ikiwa hawawezi kujizuia, na waoe; maana ni afadhali kuoa kuliko kuwaka tamaa.
10 Mt 5:32;19:9;Mk 10:11-12;Lk 16:18Lakini wale waliokwisha kuoana nawaagiza; wala hapo si mimi, ila Bwana; mke asiachane na mumewe; 11 lakini, ikiwa ameachana naye, na akae asiolewe, au apatane na mumewe; tena mume asimwache mkewe.