Wake na waume
1 Efe 5:22;Kol 3:18;Tit 2:5Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 1 Pet 2:12wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 1 Tim 2:9;Isa 3:18-24Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6 Mwa 18:12;Mit 3:25Kama vile Sara alivyomtii Abrahamu, akamwita bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, pasipo kutishwa na hofu yoyote.