Publicidade

1 Pedro 3

Wake na waume

1 Efe 5:22;Kol 3:18;Tit 2:5 Kadhalika ninyi wake, watiini waume zenu; kusudi, ikiwa wako wasioliamini Neno, wavutwe kwa mwenendo wa wake zao, pasipo lile Neno; 2 1 Pet 2:12 wakiutazama mwenendo wenu safi, na wa hofu. 3 1 Tim 2:9;Isa 3:18-24 Kujipamba kwenu, kusiwe kujipamba kwa nje, yaani, kusuka nywele; na kujitia dhahabu, na kuvalia mavazi; 4 bali kuwe utu wa moyoni usioonekana, katika mapambo yasiyoharibika; yaani, roho ya upole na utulivu, iliyo ya thamani kuu mbele za Mungu. 5 Maana hivyo ndivyo walivyojipamba wanawake watakatifu wa zamani, waliomtumaini Mungu, na kuwatii waume zao. 6 Mwa 18:12;Mit 3:25 Kama vile Sara alivyomtii Abrahamu, akamwita bwana; nanyi ni watoto wake, mfanyapo mema, pasipo kutishwa na hofu yoyote. 7 Efe 5:25;Kol 3:19 Kadhalika ninyi waume, kaeni na wake zenu kwa akili; na kumpa mke heshima, kama chombo kisicho na nguvu; maana wao pia ni warithi wa neema ya uzima, ili maombi yenu yasizuiliwe na chochote.

Mateso kwa ajili ya kutenda Haki

8 Rum 12:16 Neno la mwisho ni hili; muwe na nia moja, wenye kuhurumiana, wenye kupendana kama ndugu, wasikitikivu, wanyenyekevu; 9 Zab 34:12-16;Yak 1:26;Mt 5:44;1 The 5:15;1 Pet 2:23 watu wasiolipa baya kwa baya, au laumu kwa laumu; bali wenye kubariki; kwa sababu hayo ndiyo mliyoitiwa ili mrithi baraka. 10 Zab 34:12-16;Yak 1:26 Kwa maana,

Atakaye kupenda maisha,

Na kuona siku njema,

Auzuie ulimi wake usinene mabaya,

Na midomo yake isiseme uongo.

11 Na aache mabaya, atende mema;

Atafute amani, aifuate sana.

12 Kwa kuwa macho ya Bwana huwaelekea wenye haki,

Na masikio yake husikiliza maombi yao;

Bali uso wa Bwana uko juu ya watenda mabaya.

13 Naye ni nani atakayewadhuru, mkiwa wenye juhudi katika mema? 14 Mt 5:10;Isa 8:12-13;1 Pet 2:20 Lakini hata mkiteswa kwa sababu ya kutenda haki, mna heri. Msiogope kutisha kwao, wala msifadhaike; bali mtakaseni Kristo Bwana mioyoni mwenu. 15 Isa 8:13;Kol 4:6;1 Pet 1:3,13 Muwe tayari siku zote kumjibu kila mtu awaulizaye habari za tumaini lililo ndani yenu; lakini kwa upole na kwa heshima. 16 1 Pet 2:12 Nanyi muwe na dhamiri njema, ili katika neno lile mnalosingiziwa, watahayarishwe wale wautukanao mwenendo wenu mwema katika Kristo. 17 1 Pet 2:20-24 Maana ni afadhali kuteswa kwa kutenda mema, ikiwa ndiyo mapenzi ya Mungu, kuliko kwa kutenda mabaya. 18 Rum 6:10;Efe 2:18;Ebr 9:28;10:10 Kwa maana Kristo naye aliteswa mara moja kwa ajili ya dhambi, mwenye haki kwa ajili yao wasio haki, ili atulete kwa Mungu; akauawa kimwili, lakini akahuishwa kiroho, 19 1 Pet 4:8 ambayo kwa hiyo aliwaendea roho waliokaa kifungoni, akawahubiria; 20 Mwa 6:1—7:7,17,24 watu wasiotii hapo zamani, wakati Mungu alipowavumilia kwa subira, siku za Nuhu, safina ilipokuwa ikitengenezwa; ambamo ndani yake wachache, yaani, watu wanane, waliokoka kwa maji. 21 Efe 5:26;Ebr 10:22 Mfano wa mambo hayo ni ubatizo, unaowaokoa ninyi pia siku hizi; (siyo kuwekea mbali uchafu wa mwili, bali jibu la dhamiri safi mbele za Mungu), kwa kufufuka kwake Yesu Kristo. 22 Efe 1:20,21;Zab 110:1;Kol 1:16 Naye yuko katika mkono wa kulia wa Mungu, amekwenda zake mbinguni, malaika na enzi na nguvu zikiisha kutiishwa chini yake.

Veja também

Bíblia Online Bíblia Online

Bíblia Online • Versão: 2026-07-04_21-26-40-