9 Mit 15:27;1 Tim 6:10Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.
20 Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.
22 Zab 50:8,9;Mit 21:3;Isa 1:11;Yer 7:22;Amo 5:21,24;Mik 6:6;Mt 9:13;12:7;Ebr 10:6;Kut 19:5;Mhu 5:1;Yer 7:23;Hos 6:6;Mt 5:24;9:13;Mk 12:33Naye Samweli akasema,
Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu
Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?
Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,
Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.
23 Kum 18:10Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,
Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;
Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,
Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.