Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 15:9,20-23

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi, na kondoo na ng’ombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona, na kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

20 Sauli akasema, "Lakini nilimtii Mwenyezi Mungu. Nilikamilisha ile kazi ambayo Mwenyezi Mungu alinituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao. 21 Askari walichukua kondoo na ng’ombe kutoka nyara, kutoka kwa wale wazuri sana katika vitu vilivyotengewa Mungu, ili wavitoe kuwa dhabihu kwa Mwenyezi Mungu, Mungu wako, huko Gilgali."

22 Lakini Samweli akajibu:

"Je, Mwenyezi Mungu anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

kama vile kuitii sauti ya Mwenyezi Mungu?

Kutii ni bora kuliko dhabihu,

nako kusikia ni bora

kuliko mafuta ya kondoo dume.

23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

Kwa sababu umelikataa neno la Mwenyezi Mungu,

naye amekukataa wewe

kuendelea kuwa mfalme."

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    9 Mit 15:27;1 Tim 6:10Lakini Sauli na watu wake wakamwacha Agagi hai, na katika kondoo walio wazuri, na ng’ombe, na vinono, na wana-kondoo, na chochote kilicho chema, wala hawakukubali kuwaangamiza; bali chochote kilichokuwa kibaya na kisichofaa, ndicho walichoangamiza kabisa.

    20 Sauli akamwambia Samweli, Hakika mimi nimeitii sauti ya BWANA, nami nimemleta Agagi, mfalme wa Waamaleki, tena nimewaangamiza Waamaleki kabisa. 21 Ila watu waliteka nyara, kondoo na ng’ombe walio wazuri, katika vitu vilivyowekwa wakfu, kusudi wavitoe dhabihu kwa BWANA, Mungu wako, huko Gilgali.

    22 Zab 50:8,9;Mit 21:3;Isa 1:11;Yer 7:22;Amo 5:21,24;Mik 6:6;Mt 9:13;12:7;Ebr 10:6;Kut 19:5;Mhu 5:1;Yer 7:23;Hos 6:6;Mt 5:24;9:13;Mk 12:33Naye Samweli akasema,

    Je! BWANA huzipenda sadaka za kuteketezwa na dhabihu

    Sawasawa na kuitii sauti ya BWANA?

    Angalia, kutii ni bora kuliko dhabihu,

    Na kusikiza ushauri kuliko mafuta ya beberu.

    23 Kum 18:10Kwani kuasi ni kama dhambi ya uchawi,

    Na ukaidi ni kama uovu na kuabudu vinyago;

    Kwa kuwa umelikataa neno la BWANA,

    Yeye naye amekukataa wewe usiwe mfalme.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    9 Lakini Sauli na hilo jeshi wakamhifadhi hai Agagi na kondoo na ngʼombe walio wazuri, mafahali na wana-kondoo walionona kila kitu kilichokuwa kizuri. Hivi vitu hawakuwa radhi kuviangamiza kabisa, bali kila kitu kilichodharauliwa na kilicho dhaifu wakakiangamiza kabisa.

    20 Sauli akasema, "Lakini nilimtii Bwana. Nilikamilisha ile kazi ambayo Bwana alinituma. Niliwaangamiza Waamaleki kabisa na kumleta Agagi mfalme wao. 21 Askari walichukua kondoo na ngʼombe kutoka kwenye nyara, zile ambazo ni nzuri sana zimewekwa wakfu kwa Mungu, ili zitolewe dhabihu kwa Bwana Mungu wako huko Gilgali."

    22 Lakini Samweli akajibu:

    "Je, Bwana anafurahia sadaka za kuteketezwa na dhabihu

    kama vile kuitii sauti ya Bwana?

    Kutii ni bora zaidi kuliko dhabihu,

    nako kusikia ni bora

    kuliko mafuta ya kondoo dume.

    23 Kwa maana kuasi ni kama dhambi ya uaguzi,

    nao ukaidi ni kama uovu wa kuabudu sanamu.

    Kwa sababu umelikataa neno la Bwana,

    naye amekukataa wewe

    kuendelea kuwa mfalme."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.