Ombi la Hana
1 Lk 1:46-55;Flp 4:6;Zab 9:14;13:5;20:5Naye Hana akaomba, akasema,
Moyo wangu wamshangilia BWANA,
Pembe yangu imetukuka katika BWANA,
Kinywa changu kimepanuka juu ya adui zangu;
Kwa kuwa naufurahia wokovu wako;
2 Kut 15:11;Isa 6:3;57:15;Kum 4:35;Zab 73:25Hakuna aliye mtakatifu kama BWANA;
Kwa maana hakuna yeyote ila wewe,
Wala hakuna mwamba kama Mungu wetu.
3 Mal 3:13Msizidi kunena kwa kutakabari hivyo;
Majivuno yasitoke vinywani mwenu;
Kwa kuwa BWANA ni Mungu wa maarifa,
Naye huyapima matendo kwa mizani.
4 Pinde zao mashujaa zimevunjika,
Na hao waliojikwaa wamepata nguvu.
5 Lk 1:53;Zab 113:9;Isa 54:1;Gal 4:27Walioshiba wamejikodisha ili kupata chakula,
Lakini waliokuwa na njaa sasa hawana njaa tena.
Naam, huyo aliyekuwa tasa amezaa watoto saba,
lakini aliye na watoto wengi amehuzunika.
6 Kum 32:39;Ayu 5:18;Hos 6:1;Yn 5:25-29;11:25,26;Ufu 1:18BWANA huua, naye hufanya kuwa hai;
Hushusha hadi kuzimu, tena huleta juu.
7 Ayu 1:21;5:11;Zab 102:10;75:7BWANA hufukarisha mtu, na hutajirisha;
Hushusha chini, tena huinua juu.
8 Dan 4:17;Mwa 41:14;1 Sam 15:17;Ayu 36:7;Yak 2:5;Ufu 1:6;3:21;Ebr 1:3Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Humpandisha mhitaji kutoka jaani,
Ili awaketishe pamoja na wakuu,
Wakakirithi kiti cha enzi cha utukufu;
Kwa maana nguzo za dunia zina BWANA,
Naye ameuweka ulimwengu juu yake.
9 Zab 91:11;1 Sam 14:6Yeye atailinda miguu ya watakatifu wake;
Bali waovu watanyamazishwa gizani,
Maana kwa nguvu hakuna atakayeshinda;
10 Zab 96:13Washindanao na BWANA watapondwa kabisa;
Toka mbinguni yeye atawapigia radi;
BWANA ataihukumu dunia yote;
Naye atampa mfalme wake nguvu,
Na kuitukuza pembe ya masihi2:10 Neno hili masihi, kwa Kiebrania, maana yake ni Mtiwa mafuta, au, Mwenye kuwekwa wakfu kwa kutiwa mafuta ili awe mfalme, au kuhani, au nabii. Kwa Kigiriki ni Kristo. wake.