Daudi akimbilia Gathi
10 Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi. 11 1 Sam 18:7;29:5Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,
Sauli amewaua elfu zake,
Na Daudi makumi elfu yake.
12 Zab 56:1Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi. 13 Zab 34:1Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakunakuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake. 14 Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mnaona ya kuwa mtu huyu ana wazimu; basi, maana yake nini kumleta kwangu? 15 Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe huyu ili aoneshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?