Pular para o conteúdo
Publicidade

1 Samweli 21:10-15

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Daudi huko Gathi

10 Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 11 Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, "Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:

" ‘Sauli amewaua elfu zake,

naye Daudi makumi elfu yake’?"

12 Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 13 Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango, na kuachia mate kutiririka kwenye ndevu zake.

14 Akishi akawaambia watumishi wake, "Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu? 15 Je, mimi nimepungukiwa na wenda wazimu kiasi kwamba mmeniletea mtu huyo hapa aendelee kufanya hivi mbele yangu? Je, ilikuwa ni lazima mtu huyo aje nyumbani mwangu?"

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    10 Basi Daudi akaondoka, akakimbia siku ile, kwa hofu ya Sauli, akamwendea Akishi, mfalme wa Gathi. 11 1 Sam 18:7;29:5Nao watumishi wa Akishi wakamwambia, Je! Huyu siye yule Daudi, mfalme wa nchi? Je! Hawakuimbiana habari zake katika ngoma zao, kusema,

    Sauli amewaua elfu zake,

    Na Daudi makumi elfu yake.

    12 Zab 56:1Naye Daudi akayatia maneno hayo moyoni mwake, akamwogopa sana Akishi, mfalme wa Gathi. 13 Zab 34:1Akaubadilisha mwenendo wake mbele yao, akajifanya mwenye wazimu mikononi mwao, akakunakuna katika mbao za mlango, na kuyaacha mate yake kuanguka juu ya ndevu zake. 14 Ndipo huyo Akishi akawaambia watumishi wake, Angalieni, mnaona ya kuwa mtu huyu ana wazimu; basi, maana yake nini kumleta kwangu? 15 Je! Mimi nina haja ya watu wenye wazimu, hata mmemleta kiumbe huyu ili aoneshe wazimu wake machoni pangu? Je! Huyu ataingia nyumbani mwangu?

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    10 Siku ile Daudi akamkimbia Sauli na kwenda kwa Akishi mfalme wa Gathi. 11 Lakini watumishi wa Akishi wakamwambia, "Je, huyu si ndiye Daudi mfalme wa nchi? Je, huyu si ndiye yule ambaye wanaimba katika ngoma zao wakisema:

    " ‘Sauli amewaua elfu zake,

    naye Daudi makumi elfu yake’?"

    12 Daudi akayaweka maneno haya moyoni naye akamwogopa sana Akishi mfalme wa Gathi. 13 Basi akajifanya mwendawazimu mbele yao; naye alipokuwa mikononi mwao, alitenda kama kichaa, akikwaruza kwa kutia alama juu ya milango ya lango na kuachia udelele kutiririka kwenye ndevu zake.

    14 Akishi akawaambia watumishi wake, "Tazameni mtu huyu! Ana wazimu! Kwa nini mnamleta kwangu? 15 Je, mimi nimepungukiwa na wenda wazimu kiasi kwamba mmeniletea mtu huyo hapa aendelee kufanya hivi mbele yangu? Je, ilikuwa ni lazima mtu huyo aje nyumbani kwangu?"

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.