Onyo juu ya waalimu waongo
3 Mdo 20:1Kama vile nilivyokusihi ukae Efeso, nilipokuwa nikisafiri kwenda Makedonia, ili uwakataze wengine wasifundishe elimu nyingine; 4 1 Tim 4:7wala wasiangalie hadithi na nasaba zisizo na kikomo, zinazozua maswali wala si mpango1:4 ‘Mpango’ katika Kigiriki ni ‘uwakili’. wa Mungu ulio katika imani; basi uwaambie hivyo. 5 Rum 13:10;Gal 5:6Lakini lengo la agizo hili ni kuleta upendo utokao katika moyo safi na dhamiri njema, na imani isiyo na unafiki. 6 1 Tim 6:4,20Wengine wakiyakosa hayo wamegeukia maneno ya ubatili; 7 wakitaka kuwa waalimu wa sheria, ingawa hawayafahamu wasemayo wala mambo yale wayanenayo kwa uthabiti.