1 2 The 3:6 Iliyobaki, ndugu, tunawasihi na kuwaonya kwamba mwenende katika Bwana Yesu; kama mlivyopokea kwetu jinsi iwapasavyo kuenenda na kumpendeza Mungu, kama nanyi mnavyoenenda, vivyo hivyo mpate kuzidi sana. 2 Kwa kuwa mnajua ni maagizo gani tuliyowapa kwa Bwana Yesu. 3 1 The 5:23;Ebr 10:10;1 Pet 1:16 Maana haya ndiyo mapenzi ya Mungu, kutakaswa kwenu, mwepukane na uasherati; 4 1 Kor 6:13,15 kila mmoja wenu ajue kuuweza mwili wake katika utakatifu na heshima; 5 Yer 10:25;Zab 79:6 si katika hali ya tamaa mbaya, kama Mataifa wasiomjua Mungu. 6 Zab 94:2 Mtu asimpunje ndugu yake wala kumkosea katika jambo hili; kwa sababu Bwana ndiye alipizaye kisasi cha haya yote; kama tulivyowaambia kwanza, tukashuhudia sana. 7 2 The 2:13,14 Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. 8 Lk 10:16;Eze 36:27;37:14 Basi yeye anayekataa, hakatai mwanadamu bali Mungu, anayewapa ninyi Roho wake Mtakatifu.
9 Yn 13:34;Yer 31:33,34 Kuhusu upendano, hamna haja niwaandikie; maana ninyi wenyewe mmefundishwa na Mungu kupendana. 10 2 The 3:4 Kwa maana mnafanya neno hili kwa ndugu wote walio katika Makedonia yote. Lakini tunawasihi, ndugu, mzidi sana. 11 Efe 4:28;2 The 3:8,12 Tena mjitahidi kutulia, na kutenda shughuli zenu, na kufanya kazi kwa mikono yenu wenyewe, kama tulivyowaagiza; 12 Kol 4:5;1 Kor 5:12,13 ili mwende kwa adabu mbele yao walio nje, wala msiwe na haja ya kitu chochote.
13 1 Kor 15:20;Efe 2:12 Lakini, ndugu, hatutaki msijue habari zao waliolala mauti, msije mkahuzunika kama na wengine wasio na matumaini. 14 Rum 14:9;1 Kor 15:3,4,12 Maana, ikiwa tunaamini ya kwamba Yesu alikufa akafufuka, vivyo hivyo na hao waliolala katika Yesu, Mungu atawaleta pamoja naye. 15 1 Kor 15:51-52;7:10,25 Kwa kuwa tunawaambieni haya kwa neno la Bwana, kwamba sisi tulio hai, tutakaosalia hata wakati wa kuja kwake Bwana, hakika hatutawatangulia wao waliokwisha kulala mauti. 16 1 Kor 15:52;2 The 1:7 Kwa sababu Bwana mwenyewe atashuka kutoka mbinguni pamoja na mwaliko, na sauti ya malaika mkuu, na parapanda ya Mungu; nao waliokufa katika Kristo watafufuliwa kwanza. 17 Yn 12:26;17:24 Kisha sisi tulio hai, tuliosalia, tutanyakuliwa pamoja nao katika mawingu, ili tumlaki Bwana hewani; na hivyo tutakuwa pamoja na Bwana milele. 18 Basi, farijianeni kwa maneno hayo.