20 Ufu 3:14Maana ahadi zote za Mungu zilizopo katika yeye ni Ndiyo; tena kwa hiyo katika yeye ni Amin; Mungu apate kutukuzwa kwa sisi. 21 1 Yoh 2:27Basi Yeye atufanyaye imara pamoja nanyi katika Kristo, na kututia mafuta, ni Mungu, 22 2 Kor 5:5;Rum 8:16;Efe 1:13,14naye ndiye aliyetutia mhuri akatupa arabuni ya Roho mioyoni mwetu.