Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Coríntios 6

1 2 Kor 1:24;5:20 Nasi tukitenda kazi pamoja naye twawasihi msiipokee neema ya Mungu bure. 2 Isa 49:8;Lk 4:19,21 (Kwa maana asema,

Kwa wakati uliokubalika nilikusikia,

Na katika siku ya wokovu nilikusaidia;

tazama, wakati uliokubalika ndio sasa; tazama, siku ya wokovu ndiyo sasa.) 3 Tusiwe kwazo la namna yoyote katika jambo lolote, ili utumishi wetu usilaumiwe; 4 2 Kor 4:2 bali katika kila neno tujipatie sifa njema, kama watumishi wa Mungu; katika subira nyingi, katika mateso, katika shida, katika matatizo; 5 Mdo 16:23;2 Kor 11:23-27 katika mapigo, katika vifungo, katika fitina, katika taabu, katika kukesha, katika kufunga; 6 1 Tim 4:12 katika kuwa safi, katika elimu, katika uvumilivu, katika utu wema, katika Roho Mtakatifu, katika upendo usio unafiki; 7 1 Kor 2:4 katika neno la kweli, katika nguvu ya Mungu; kwa silaha za haki za mkono wa kulia na za mkono wa kushoto; 8 kwa utukufu na aibu; kwa kunenwa vibaya na kunenwa vema; kama wadanganyao, bali tu watu wa kweli; 9 2 Kor 4:10;Zab 118:18 kama wasiojulikana, bali wajulikanao sana; kama wanaokufa, kumbe tu hai; kama wanaorudiwa, bali wasiouawa; 10 Flp 4:12,13 kama wenye huzuni, bali siku zote tu wenye furaha; kama maskini, bali tukitajirisha wengi; kama wasio na kitu, bali tu wenye vitu vyote.

11 Zab 119:32 Vinywa vyetu vimefumbuliwa kwenu, enyi Wakorintho; mioyo yetu imekunjuliwa. 12 Hamsongwi ndani yetu, bali mwasongwa katika mioyo yenu. 13 1 Kor 4:14 Basi, ili mlipe kadiri ile mliyopewa (nasema nanyi kama na watoto), nanyi pia mkunjuliwe mioyo.

Hekalu la Mungu aliye hai

14 Efe 5:11 Msifungiwe nira pamoja na wasioamini, kwa jinsi isivyo sawasawa; kwa maana pana urafiki gani kati ya haki na uasi? Tena pana shirika gani kati ya nuru na giza? 15 Tena pana ulinganifu gani kati ya Kristo na Beliari?6:15 Beliari: maana yake ni, Ufisadi. Au yeye aaminiye ana sehemu gani pamoja na yeye asiyeamini? 16 Law 26:12;Eze 37:27;1 Kor 3:16;6:19;Eze 37:27 Tena pana mapatano gani kati ya hekalu la Mungu na sanamu? Kwa maana sisi tu hekalu la Mungu aliye hai; kama Mungu alivyosema, ya kwamba, Nitakaa ndani yao, na kati yao nitatembea, nami nitakuwa Mungu wao, nao watakuwa watu wangu. 17 Isa 52:11;Yer 51:45;Eze 20:34,41;Ufu 18:4 Kwa hiyo,

Tokeni kati yao,

Mkatengwe nao, asema Bwana,

Msiguse kitu kilicho kichafu,

Nami nitawakaribisha.

18 2 Sam 7:8,14;1 Nya 17:13;Isa 43:6;Yer 31:9;32:38;Hos 1:10;Amo 4:13 Nitakuwa Baba kwenu,

Nanyi mtakuwa kwangu wanangu wa kiume na wa kike,

asema Bwana Mwenyezi.

Veja também