Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Samweli 16:5,7,10-12

SRUV Swahili Revised Union Version

Shimei amlaani Daudi

5 2 Sam 19:16;1 Fal 2:8Basi mfalme Daudi alipofika Bahurimu, tazama, kulitoka huko mtu wa jamaa ya nyumba ya Sauli, jina lake akiitwa Shimei, mwana wa Gera; alitoka, akalaani alipokuwa akienda. 7 Na Shimei alipolaani, alisema hivi, Nenda zako! Nenda zako! Ewe mtu wa damu! Ewe mtu usiyefaa! 10 2 Sam 3:39;19:22;1 Pet 2:23;2 Fal 18:25;Omb 3:38;Rum 9:20Mfalme akasema, Nina nini na ninyi, enyi wana wa Seruya? Kwa sababu yeye analaani, na kwa sababu BWANA amemwambia, Mlaani Daudi, basi, ni nani atakayesema, Mbona umetenda haya? 11 Daudi akamwambia Abishai, na watumishi wake wote, Angalieni, huyu mwanangu, aliyetoka viunoni mwangu, anautafuta uhai wangu; sembuse Mbenyamini huyu? Mwacheni alaani, kwa sababu BWANA ndiye aliyemwagiza. 12 Mwa 29:32;1 Sam 1:11;Zab 25:18;37:7;Yer 24:5-7;Omb 3:22-26;Mt 5:11,12;Rum 8:28;2 Kor 4:17Labda BWANA atayaangalia mabaya yaliyonipata, naye BWANA atanilipa mema kwa sababu ya kunilaani kwake leo.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    5 Mfalme Daudi alipokuwa anakaribia Bahurimu, mtu mmoja wa ukoo wa jamaa ya Sauli, akatoka humo. Jina lake ni Shimei mwana wa Gera; akawa analaani alipokuwa akitoka. 7 Shimei alivyokuwa akilaani, akasema, "Toka hapa, toka hapa, wewe mtu wa damu, wewe mtu mbaya kabisa!

    10 Lakini mfalme akamwambia, "Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Mwenyezi Mungu amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ "

    11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, "Mwanangu, ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuniua. Je, si zaidi sana huyu Mbenyamini! Mwacheni; acha alaani, kwa maana Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo. 12 Inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo."

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Mfalme Daudi alipokuwa anakaribia Bahurimu, mtu mmoja kutoka ukoo huo huo kama jamaa ya Sauli, akatoka humo, ambaye jina lake ni Shimei mwana wa Gera; akawa analaani alipokuwa akitoka. 7 Shimei alivyokuwa akilaani, akasema, "Toka hapa, toka hapa, wewe mtu wa damu, wewe mtu mbaya kabisa!

    10 Lakini mfalme akamwambia, "Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Bwana amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ "

    11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, "Mwanangu, yeye ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuuondoa uhai wangu. Je, si zaidi sana kwa huyu Mbenyamini! Mwacheni, acha alaani, kwa maana Bwana amemwambia afanye hivyo. 12 Inawezekana kwamba Bwana ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo."

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.