Shimei amlaani Daudi
5 Mfalme Daudi alipokuwa anakaribia Bahurimu, mtu mmoja wa ukoo wa jamaa ya Sauli, akatoka humo. Jina lake ni Shimei mwana wa Gera; akawa analaani alipokuwa akitoka. 7 Shimei alivyokuwa akilaani, akasema, "Toka hapa, toka hapa, wewe mtu wa damu, wewe mtu mbaya kabisa!
10 Lakini mfalme akamwambia, "Mna nini nami, enyi wana wa Seruya? Ikiwa analaani kwa sababu Mwenyezi Mungu amemwambia, ‘Mlaani Daudi,’ nani awezaye kuuliza, ‘Kwa nini unafanya hivi?’ "
11 Ndipo Daudi akamwambia Abishai na maafisa wake wote, "Mwanangu, ambaye ametoka viunoni mwangu mwenyewe, anajaribu kuniua. Je, si zaidi sana huyu Mbenyamini! Mwacheni; acha alaani, kwa maana Mwenyezi Mungu amemwambia afanye hivyo. 12 Inawezekana kwamba Mwenyezi Mungu ataona dhiki yangu na kunilipa mema kwa ajili ya laana ninayopokea leo."