Pular para o conteúdo
Publicidade

2 Samweli 5

Daudi atiwa mafuta kuwa mfalme wa Israeli

1 1 Nya 12:23;Mwa 29:14Ndipo watu wa kabila zote za Israeli wakamwendea Daudi huko Hebroni, wakasema naye, wakinena, Tazama, sisi tu mfupa wako na nyama yako. 2 1 Sam 18:13;16:1;2 Sam 7:7;Zab 78:71Zamani za kale, hapo Sauli alipokuwa mfalme juu yetu, wewe ndiwe uliyewaongoza Israeli wakitoka nje kwenda, na kurudi vitani. Naye BWANA akakuambia, Wewe utawalisha watu wangu Israeli, nawe utakuwa mkuu juu ya Israeli. 3 1 Nya 11:3;2 Fal 11:17;Amu 11:11;1 Sam 23:18Basi wazee wote wa Israeli wakamwendea mfalme huko Hebroni, naye mfalme Daudi akapatana nao huko Hebroni mbele za BWANA; wakamtia Daudi mafuta awe mfalme juu ya Israeli.

Veja também