15 Yn 5:39;Zab 119:99na ya kuwa tangu utotoni umeyajua Maandiko Matakatifu, ambayo yaweza kukuhekimisha hata upate wokovu kwa imani iliyo katika Kristo Yesu. 16 2 Pet 1:19-21;Rum 15:4Kila andiko, lenye pumzi ya Mungu, lafaa kwa mafundisho, na kwa kuwaonya watu makosa yao, na kwa kuwaongoza, na kwa kuwaadibisha katika haki; 17 1 Tim 6:11ili mtu wa Mungu awe kamili, amekamilishwa apate kutenda kila tendo jema.