Ujumbe wa Sardi
1 Ufu 5:6;1:16Na kwa malaika wa kanisa lililoko Sardi andika; Haya ndiyo anenayo yeye aliye na hizo Roho saba za Mungu, na zile nyota saba. Nayajua matendo yako, ya kuwa una jina la kuwa hai, nawe umekufa. 2 Eze 34:4Uwe mwenye kukesha, ukayaimarishe mambo yaliyobakia, yanayotaka kufa. Maana sikuona matendo yako kuwa yametimilika mbele za Mungu wangu.