Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 5:1-6

SRUV Swahili Revised Union Version

Kitabu na Mwana-kondoo

1 Eze 2:9-10;Isa 6:1;29:11;Zab 47:8;Ufu 4:2Kisha nikaona katika mkono wa kulia wake yeye aliyeketi juu ya kile kiti cha enzi kitabu kilichoandikwa ndani na nyuma, kimetiwa mihuri saba. 2 Nikaona malaika mwenye nguvu akihubiri kwa sauti kuu, Ni nani anayestahili kukifungua kitabu, na kuivunja mihuri yake? 3 Wala hapakuwa na mtu mbinguni, wala juu ya nchi, wala chini ya nchi, aliyeweza kukifungua kitabu hicho, wala kukitazama. 4 Nami nikalia sana kwa kuwa hapakuonekana mtu astahiliye kukifungua kitabu hicho, wala kukitazama. 5 Mwa 49:9;Isa 11:1,10;Ufu 22:16Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba. 6 Isa 53:7;11:2;Yn 1:29,36;Ufu 4:5;Zek 4:10Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    1 Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na nje, kikiwa kimefungwa kwa mihuri saba. 2 Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, "Ni nani anayestahili kuivunja hiyo mihuri na kukifungua kitabu?" 3 Lakini hapakuwa na yeyote mbinguni wala duniani au chini ya dunia aliyeweza kukifungua hicho kitabu, wala hata kutazama ndani yake. 4 Nikalia sana kwa sababu hakuonekana yeyote anayestahili kukifungua hicho kitabu wala kutazama ndani yake. 5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba."

    6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba5:6 Roho saba za Mwenyezi Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu zilizotumwa duniani pote.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    1 Kisha nikaona katika mkono wake wa kuume wa yule aliyeketi kwenye kile kiti cha enzi, kitabu kilichoandikwa ndani na upande wa nje, kikiwa kimefungwa kwa lakiri saba. 2 Nami nikamwona malaika mwenye nguvu akitangaza kwa sauti kuu, akisema, "Ni nani anayestahili kuzivunja hizo lakiri na kukifungua kitabu?" 3 Lakini hapakuwa na yeyote mbinguni wala duniani au chini ya dunia aliyeweza kukifungua hicho kitabu wala hata kutazama ndani yake. 4 Nikalia sana sana kwa sababu hakuonekana yeyote anayestahili kukifungua hicho kitabu wala kutazama ndani yake. 5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba."

    6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba5:6 Roho saba za Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu zilizotumwa duniani pote.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.