Pular para o conteúdo
Publicidade

Ufunuo 5:5,6,9

SRUV Swahili Revised Union Version

5 Mwa 49:9;Isa 11:1,10;Ufu 22:16Na mmojawapo wa wale wazee akaniambia, Usilie; tazama, Simba aliye wa kabila la Yuda, Shina la Daudi, yeye ameshinda apate kukifungua kile kitabu, na ile mihuri yake saba. 6 Isa 53:7;11:2;Yn 1:29,36;Ufu 4:5;Zek 4:10Nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-kondoo amesimama, alikuwa kana kwamba amechinjwa, mwenye pembe saba na macho saba, ambazo ni Roho saba za Mungu zilizotumwa katika dunia yote. 9 Zab 33:3;98:1;144:9;Isa 42:10Nao waimba wimbo mpya wakisema, Wastahili wewe kukitwaa hicho kitabu na kuifungua mihuri yake; kwa kuwa ulichinjwa, ukawa fidia kwa Mungu na kwa damu yako watu wa kila kabila na lugha na jamaa na taifa,

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba."

    6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba5:6 Roho saba za Mwenyezi Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu zilizotumwa duniani pote. 9 Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema:

    "Wewe unastahili kukitwaa kitabu

    na kuivunja mihuri yake,

    kwa sababu ulichinjwa,

    na kwa damu yako ukamnunulia Mungu

    watu kutoka kila kabila, kila lugha,

    kila jamaa na kila taifa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja hizo lakiri zake saba."

    6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne na miongoni mwa wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba5:6 Roho saba za Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu zilizotumwa duniani pote. 9 Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema:

    "Wewe unastahili kukitwaa kitabu

    na kuzivunja lakiri zake,

    kwa sababu ulichinjwa

    na kwa damu yako ukamnunulia Mungu watu

    kutoka kila kabila, kila lugha,

    kila jamaa na kila taifa.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.