5 Kisha, mmoja wa wale wazee akaniambia, "Usilie! Tazama, Simba wa kabila la Yuda, wa Uzao wa Daudi, ameshinda. Yeye ndiye anayeweza kukifungua hicho kitabu na kuvunja mihuri yake saba."
6 Ndipo nikaona katikati ya kile kiti cha enzi na wale viumbe wenye uhai wanne, na katikati ya wale wazee, Mwana-Kondoo amesimama, akiwa kama amechinjwa. Alikuwa na pembe saba na macho saba, ambazo ndizo zile Roho saba5:6 Roho saba za Mwenyezi Mungu hapa inamaanisha Roho wa Mungu katika ukamilifu wa utendaji wake. za Mungu zilizotumwa duniani pote. 9 Nao wakaimba wimbo mpya, wakisema:
"Wewe unastahili kukitwaa kitabu
na kuivunja mihuri yake,
kwa sababu ulichinjwa,
na kwa damu yako ukamnunulia Mungu
watu kutoka kila kabila, kila lugha,
kila jamaa na kila taifa.