Pular para o conteúdo
Publicidade

Matendo 8:30-35

SRUV Swahili Revised Union Version

30 Basi Filipo akaenda mbio, akamsikia anasoma kitabu cha nabii Isaya; akanena, Je! Yamekuelea haya unayosoma? 31 Yn 16:13Akasema, Nitawezaje kuelewa, mtu asiponiongoza? Akamsihi Filipo apande na kuketi pamoja naye. 32 Isa 53:7-8Na fungu la Maandiko alilokuwa akilisoma ni hili,

Aliongozwa kwenda machinjoni kama kondoo,

Na kama vile mwana-kondoo alivyo kimya mbele yake yule amkataye manyoya,

Vivyo hivyo yeye naye hafunui kinywa chake.

33 Katika kujidhili kwake hukumu yake iliondolewa.

Ni nani atakayeeleza kizazi chake?

Kwa maana uzima wake umeondolewa katika nchi.

34 Yule towashi akamjibu Filipo, akasema, Nakuomba, nabii huyu; asema maneno haya kwa habari ya nani; ni habari zake mwenyewe au za mtu mwingine? 35 Filipo akafunua kinywa chake, naye, akianza kwa andiko lilo hilo, akamhubiria Habari Njema za Yesu.

Em outras traduções

  1. ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

    30 Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, "Je, unaelewa hayo unayoyasoma?"

    31 Yule towashi akasema, "Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?" Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.

    32 Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko:

    "Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,

    kama mwana-kondoo anyamazavyo

    mbele yake yule amkataye manyoya,

    hivyo hakufungua kinywa chake.

    33 Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.

    Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?

    Kwa maana maisha yake yaliondolewa

    kutoka duniani."

    34 Yule towashi akamuuliza Filipo, "Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?" 35 Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza Injili ya Isa.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    30 Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, "Je, unaelewa hayo usomayo?"

    31 Yule towashi akasema, "Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?" Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.

    32 Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko:

    "Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,

    kama mwana-kondoo anyamazavyo

    mbele yake yule amkataye manyoya,

    hivyo hakufungua kinywa chake.

    33 Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.

    Nani awezaye kueleza juu ya kizazi chake?

    Kwa maana maisha yake yaliondolewa

    kutoka duniani."

    34 Yule towashi akamuuliza Filipo, "Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?" 35 Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza habari njema za Yesu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.