30 Ndipo Filipo akakimbilia lile gari na kumsikia yule mtu anasoma kitabu cha nabii Isaya. Filipo akamuuliza, "Je, unaelewa hayo unayoyasoma?"
31 Yule towashi akasema, "Nitawezaje kuelewa mtu asiponifafanulia?" Hivyo akamkaribisha Filipo ili apande na kuketi pamoja naye.
32 Huyu towashi alikuwa anasoma fungu hili la Maandiko:
"Aliongozwa kama kondoo aendaye machinjoni,
kama mwana-kondoo anyamazavyo
mbele yake yule amkataye manyoya,
hivyo hakufungua kinywa chake.
33 Katika kufedheheshwa kwake alinyimwa haki yake.
Nani awezaye kueleza kuhusu kizazi chake?
Kwa maana maisha yake yaliondolewa
kutoka duniani."
34 Yule towashi akamuuliza Filipo, "Tafadhali niambie, nabii huyu anena habari zake mwenyewe au habari za mtu mwingine?" 35 Ndipo Filipo akaanza kutumia fungu lile la Maandiko, akamweleza Injili ya Isa.