Ndoto za mapenzi
1 Zab 4:6;6:6;Isa 26:9 Usiku kitandani nilimtafuta mpendwa wa nafsi yangu,
Nilimtafuta, nisimpate.
2 Nikasema, Haya, niondoke nizunguke mjini,
Katika njia zake na viwanjani,
Nimtafute mpendwa wa nafsi yangu.
Nikamtafuta, nisimpate.
3 Wim 5:7;Isa 21:6-8,11,12 Walinzi wazungukao mjini waliniona;
Je! Mmemwona mpendwa wa nafsi yangu?
4 Mit 8:17;4:13;Rum 8:35,39 Kitambo kidogo tu nilipoachana nao,
Nikamwona mpendwa wa nafsi yangu;
Nikamshika, nisimwache tena,
Hata nilipomleta nyumbani mwa mamangu,
Chumbani mwake aliyenizaa.
5 Wim 2:7 Nawasihi, enyi binti za Yerusalemu,
Kwa paa na kwa ayala wa porini,
Msiyachochee mapenzi, wala kuyaamsha,
Hata yatakapoona vema yenyewe.
Bwana arusi na kundi lake wakaribia
6 Wim 8:5;Yer 2:2 Ni nani huyu apandaye kutoka nyikani,
Mfano wake ni nguzo za moshi;
Afukizwa manemane na ubani,
Na mavumbi ya manukato yote ya mchuuzi?
7 Tazama, ni machela yake Sulemani;
Mashujaa sitini waizunguka,
Wa mashujaa wa Israeli.
8 Wote wameshika upanga,
Wamehitimu kupigana;
Kila mtu anao upanga wake pajani
Kwa hofu ya kamsa za usiku.
9 Mfalme Sulemani alijitengenezea machela
Ya miti ya Lebanoni;
10 Mt 22:37;Yn 13:1,34;Rum 5:8;Efe 3:19;1 Pet 1:7,8 Nguzo zake alizitengeneza za fedha,
Na mgongo wake wa dhahabu,
Kiti chake kimepambwa urujuani,
Gari lake limenakishiwa njumu,
Hiba ya binti za Yerusalemu.
11 Ufu 11:15;Zab 110:3;Isa 62:5 Tokeni, enyi binti za Sayuni,
Mtazameni Mfalme Sulemani,
Amevaa taji alilovikwa na mamaye,
Siku ya posa yake,
Siku ya furaha ya moyo wake.