6 Isa 49:16;Yer 22:24;Hag 2:23;Flp 3:8Nitie kama mhuri moyoni mwako,
Kama mhuri juu ya mkono wako;
Kwa maana upendo una nguvu kama mauti,
Na wivu ni mkali kama ahera.
Mwako wake ni mwako wa moto,
Na miali yake ni miali ya Yahu.
7 Mit 6:35Maji mengi hayawezi kuuzimisha upendo,
Wala mito haiwezi kuuzamisha;
Kama mtu angetoa badala ya upendo
Mali yote ya nyumbani mwake,
Angedharauliwa kabisa.