1 Mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako,
Kabla hazijaja siku zilizo mbaya,
Wala haijakaribia miaka utakaposema,
Mimi sina furaha katika hiyo.
2 Kabla jua, na nuru, na mwezi,
Na nyota, havijatiwa giza;
Kabla ya kurudi mawingu baada ya mvua;
3 Zab 71:9;Zek 8:4;2 Kor 5:1;Mwa 27:1Siku ile walinzi wa nyumba watakapotetemeka;
Hapo wenye nguvu watakapojiinamisha;
Na wasagao kukoma kwa kuwa ni haba;
Na hao wachunguliao madirishani kutiwa giza;