Timotheo na Epafrodito
19 Lakini natumaini katika Bwana Yesu kumtuma Timotheo afike kwenu karibu, nifarijiwe na mimi, nikiijua hali yenu. 20 1 Kor 16:10Maana sina mtu mwingine mwenye nia moja nami, atakayeiangalia hali yenu kweli kweli. 21 2 Tim 4:10,16;Gal 4:17Maana wote wanatafuta vyao wenyewe, sivyo vya Kristo Yesu. 22 Ila mwajua sifa yake, ya kuwa ametumika pamoja nami kwa ajili ya Injili, kama mwana na baba yake.