Paulo amsifu Timotheo
19 Natumaini katika Bwana Isa kumtuma Timotheo hivi karibuni aje kwenu, ili nipate kufarijika moyo nitakapopata habari zenu. 20 Sina mtu mwingine kama yeye, ambaye ataangalia hali yenu kwa halisi. 21 Kwa maana kila mmoja anajishughulisha zaidi na mambo yake mwenyewe wala si yale ya Isa Al-Masihi. 22 Lakini ninyi wenyewe mnajua jinsi Timotheo alivyojithibitisha mwenyewe, kwa maana ametumika pamoja nami kwa kazi ya Injili, kama vile mwana kwa baba yake.