23 Hes 16:22;2 Sam 24:17;Zab 11:4-7Abrahamu akakaribia, akasema, Je! Utaharibu mwenye haki pamoja na mwovu? 24 Mt 7:13,14Huenda wakawapo wenye haki hamsini katika mji, utaharibu, wala hutauacha mji kwa ajili ya hao hamsini wenye haki waliomo? 25 Isa 3:10,11;Ayu 8:3,20;Zab 58:11;94:2;Rum 3:5,6La hasha! Usifanye hivyo, ukamwue mwenye haki pamoja na mwovu, mwenye haki awe kama mwovu. Hasha! Mhukumu ulimwengu wote asitende haki? 26 Yer 5:1;Eze 22:30;Mt 24:22BWANA akasema, Nikiona katika Sodoma wenye haki hamsini mjini, nitapaacha mahali pote kwa ajili yao.
32 Amu 6:39;Kut 34:6,7;Zab 34:15;Mit 15:29;1 Yoh 3:22;Yak 5:16Akasema, Bwana asiwe na hasira, nami nitasema mara hii tu, Huenda wakaonekana huko kumi? Akasema, Sitaharibu kwa ajili ya hao kumi. 33 Basi BWANA alipokwisha kuzungumza na Abrahamu, akaenda zake; Abrahamu naye akarudi mahali pake.