15 Hes 20:5;Zab 63:1Yale maji yalipoisha katika kiriba, Hajiri akamlaza kijana kichakani. 16 Mwa 44:34Akaenda akakaa akimkabili, mbali naye kadiri ya mtupo wa mshale; maana alisema, Nisimwone kijana akifa; naye akakaa akimkabili, akapaza sauti yake, akalia. 17 Kut 3:7;2 Fal 13:4,23Mungu akasikia sauti ya kijana. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni, akamwambia, Una nini, Hajiri? Usiogope, maana Mungu amesikia sauti ya kijana huko aliko. 19 Hes 22:31;2 Fal 6:17;Lk 24:16Mungu akamfumbua macho, naye akaona kisima cha maji; akaenda akakijaza kiriba maji, akamnywesha kijana.
Mwanzo 21:15-17,19
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, Hajiri akamwacha kijana chini ya kichaka. 16 Kisha akaenda akaketi kama umbali wa kutupa mshale, akawaza, "Siwezi kumwangalia kijana akifa." Akiwa ameketi pale, akaanza kulia kwa huzuni.
17 Mungu akamsikia kijana akilia. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni na kumwambia, "Kuna nini, Hajiri? Usiogope, Mungu amesikia kijana akilia akiwa amelala pale.
19 Ndipo Mungu akamfumbua Hajiri macho, akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, akamwacha kijana chini ya mojawapo ya vichaka. 16 Kisha akajiendea zake akaketi karibu, umbali wa kutupa mshale, akawaza, "Siwezi kumwangalia kijana akifa." Ikawa alipokuwa ameketi pale karibu, akaanza kulia kwa huzuni.
17 Mungu akamsikia kijana akilia, malaika wa Mungu akamwita Hagari kutoka mbinguni na kumwambia, "Kuna nini Hagari? Usiogope, Mungu amesikia kijana analia akiwa amelala pale.
19 Ndipo Mungu akamfumbua Hagari macho yake naye akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.