15 Maji yalipokwisha kwenye kiriba, Hajiri akamwacha kijana chini ya kichaka. 16 Kisha akaenda akaketi kama umbali wa kutupa mshale, akawaza, "Siwezi kumwangalia kijana akifa." Akiwa ameketi pale, akaanza kulia kwa huzuni.
17 Mungu akamsikia kijana akilia. Malaika wa Mungu akamwita Hajiri kutoka mbinguni na kumwambia, "Kuna nini, Hajiri? Usiogope, Mungu amesikia kijana akilia akiwa amelala pale.
19 Ndipo Mungu akamfumbua Hajiri macho, akaona kisima cha maji. Hivyo akaenda akajaza kiriba maji na kumpa kijana anywe.