Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 26

Isaka na Abimeleki

1 Mwa 12:10;20:2Ikawa njaa katika nchi hiyo, mbali na njaa ile ya kwanza iliyokuwa siku za Abrahamu. Isaka akamwendea Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, huko Gerari. 2 Mwa 12:1;Zab 37:3BWANA akamtokea, akasema, Usishuke kwenda Misri, kaa katika nchi nitakayokuambia. 3 Mwa 22:16-18;Mwa 20:1;28:15;Zab 39:12;Ebr 11:9;Mwa 12:2;13:15;Zab 105:9Kaa ugenini katika nchi hiyo, nami nitakuwa pamoja nawe, na kukubariki, maana nitakupa wewe na uzao wako nchi hizi zote. Nami nitakifanya imara kiapo nilichomwapia Abrahamu baba yako. 4 Zab 72:17Nitazidisha uzao wako kama nyota za mbinguni, nami nitawapa uzao wako nchi hizi zote, na katika uzao wako mataifa yote ya dunia watajibarikia. 5 Mwa 22:16Kwa sababu Abrahamu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. 6 Isaka akakaa katika Gerari. 7 Mwa 12:13;20:2;24:16;Mit 29:25Watu wa mahali hapo wakamwuliza habari za mkewe. Akasema, Ni dada yangu huyu maana aliogopa kusema, Ni mke wangu, watu wa nchi wasije wakamwua kwa ajili ya Rebeka; kwa maana alikuwa mzuri wa uso. 8 Ikawa alipokuwa amekaa huko siku nyingi, Abimeleki, mfalme wa Wafilisti, akachungulia dirishani, akamwona Isaka anachezacheza na Rebeka mkewe.

Veja também