16 Yn 16:21;1 Tim 2:15Akamwambia mwanamke, Hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako; kwa uchungu utazaa watoto; hata hivyo, hamu yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala. 17 Ayu 5:7;Mhu 2:23;Ebr 6:8Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nilikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako; 18 michongoma na miiba itakuzalia, nawe utakula mboga za kondeni; 19 1 Kor 15:21,22kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Mwanzo 3:16-19
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
16 Kwa mwanamke akasema,
"Nitakuzidishia sana uchungu wakati wa kuzaa kwako;
kwa uchungu utazaa watoto.
Tamaa yako itakuwa kwa mumeo,
naye atakutawala."
17 Akamwambia Adamu, "Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’
"Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako;
kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo
siku zote za maisha yako.
18 Itakuzalia miiba na mibaruti,
nawe utakula mimea ya shambani.
19 Kwa jasho la uso wako
utakula chakula chako
hadi utakaporudi ardhini,
kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo;
wewe u mavumbi
na mavumbini utarudi."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
16 Kwa mwanamke akasema,
"Nitakuzidishia sana utungu wakati wa kuzaa kwako;
kwa utungu utazaa watoto.
Tamaa yako itakuwa kwa mumeo
naye atakutawala."
17 Kwa Adamu akasema, "Kwa sababu umemsikiliza mke wako na ukala kutoka kwenye mti niliokuamuru, ‘Msile tunda lake,’
"Ardhi imelaaniwa kwa sababu yako,
kwa kazi ngumu utakula chakula kitokacho humo
siku zote za maisha yako.
18 Itazaa miiba na mibaruti kwa ajili yako,
nawe utakula mimea ya shambani.
19 Kwa jasho la uso wako
utakula chakula chako
hadi utakaporudi ardhini,
kwa kuwa ulitwaliwa kutoka humo,
kwa kuwa wewe u mavumbi
na mavumbini wewe utarudi."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.