3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa BWANA. 4 Kut 13:12;34:19;Law 27:26;Hes 18:17;Mit 3:9;Amu 6:21Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake; 5 Ebr 11:4;Mwa 3:16bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana. 6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana? 7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, lakini yapasa uishinde.
Mwanzo 4:3-7
Em outras traduções
- ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas
3 Baada ya muda, Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba ikiwa sadaka kwa Mwenyezi Mungu. 4 Lakini Habili akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Mwenyezi Mungu akamkubali Habili pamoja na sadaka yake, 5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.
6 Kisha Mwenyezi Mungu akamwambia Kaini, "Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, ikikutamani wewe, lakini inakupasa uishinde."
- ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli
3 Baada ya muda Kaini akaleta baadhi ya mazao ya shamba kama sadaka kwa Bwana. 4 Lakini Abeli akaleta fungu nono kutoka baadhi ya wazaliwa wa kwanza wa mifugo yake. Bwana akamkubali Abeli pamoja na sadaka yake, 5 lakini Mungu hakumkubali Kaini pamoja na sadaka yake. Kwa hiyo Kaini akakasirika sana, uso wake ukawa na huzuni.
6 Kisha Bwana akamwambia Kaini, "Kwa nini umekasirika? Kwa nini uso wako una huzuni? 7 Ukifanya lililo sawa, je, hutakubalika? Lakini usipofanya lililo sawa, dhambi inakuvizia mlangoni mwako, inakutamani wewe, lakini inakupasa uishinde."
Direitos das traduções citadas
Estes versículos te tocaram? Ore agora!
+581 estão orando agora.
Junte-se à corrente de oração.