Yusufu awasamehe ndugu zake
15 Ayu 15:21Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. 17 Mit 28:13;Mwa 49:25Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwasamehe ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utusamehe kosa la watumishi wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye. 19 Kum 32:35;Rum 12:19;Ebr 10:30Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? 20 Zab 56:5;Isa 10:7;Mwa 45:5,7;Mdo 3:13-15Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. 21 Mwa 47:12;Mt 5:44Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.