Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 50:15,17,19-21

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

Yusufu awaondolea ndugu zake mashaka

15 Ndugu zake Yusufu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, "Itakuwaje kama Yusufu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?" 17 ‘Hili ndilo mtakalomwambia Yusufu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako." Ujumbe huu ulipomfikia, Yusufu akalia.

19 Lakini Yusufu akawaambia, "Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? 20 Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. 21 Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu." Akawafariji na kusema nao kwa wema.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    15 Ayu 15:21Ndugu zake Yusufu walipoona ya kwamba baba yao amekufa, walisema, Labda Yusufu atatuchukia; naye atatulipa maovu yetu tuliyomtenda. 17 Mit 28:13;Mwa 49:25Mwambieni Yusufu hivi, Naomba uwasamehe ndugu zako kosa lao na dhambi yao, maana walikutenda mabaya; sasa twakuomba utusamehe kosa la watumishi wa Mungu wa baba yako. Yusufu akalia waliposema naye. 19 Kum 32:35;Rum 12:19;Ebr 10:30Yusufu akawaambia, Msiogope, je! Mimi ni badala ya Mungu? 20 Zab 56:5;Isa 10:7;Mwa 45:5,7;Mdo 3:13-15Nanyi kweli mlinikusudia mabaya, bali Mungu aliyakusudia kuwa mema, ili itokee kuokoa taifa kubwa, kama ilivyo leo. 21 Mwa 47:12;Mt 5:44Basi sasa msiogope; mimi nitawalisha na watoto wenu. Akawafariji, na kusema nao vema.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    15 Ndugu zake Yosefu walipoona kwamba baba yao amekufa, wakasema, "Itakuwaje kama Yosefu ataweka kinyongo dhidi yetu na kutulipa mabaya yote tuliyomtendea?" 17 ‘Hili ndilo mtakalomwambia Yosefu: Ninakuomba uwasamehe ndugu zako dhambi na mabaya kwa vile walivyokutenda vibaya.’ Sasa tafadhali samehe dhambi za watumishi wa Mungu wa baba yako." Ujumbe huu ulipomfikia, Yosefu akalia.

    19 Lakini Yosefu akawaambia, "Msiogope. Je, mimi ni badala ya Mungu? 20 Mlikusudia kunidhuru, lakini Mungu alikusudia mema, ili litimie hili linalofanyika sasa, kuokoa maisha ya watu wengi. 21 Hivyo basi, msiogope. Mimi nitawatunza ninyi nyote pamoja na watoto wenu." Akawahakikishia na kusema nao kwa wema.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.