5 Rum 1:28-31;Mwa 8:21;Kum 29:19;Mit 6:18;Mt 15:19;Mt 24:37;Lk 17:26;1 Pet 3:20BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 8 Mwa 19:19;Kut 33:12;Lk 1:30;Mdo 7:46Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.
13 Eze 7:2;Amo 8:2;1 Pet 4:8Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia. 14 Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu. 16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.