Pular para o conteúdo
Publicidade

Mwanzo 6:5,8,13-16

ONMM Edição Palavra Aberta: Escrituras Sagradas

5 Mwenyezi Mungu akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 8 Lakini Nuhu akapata kibali machoni pa Mwenyezi Mungu.

13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Nuhu, "Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje; tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa mia tatu6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135., upana wake dhiraa hamsini6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5., na kimo chake dhiraa thelathini6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5.. 16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

Em outras traduções

  1. SRUV Swahili Revised Union Version

    5 Rum 1:28-31;Mwa 8:21;Kum 29:19;Mit 6:18;Mt 15:19;Mt 24:37;Lk 17:26;1 Pet 3:20BWANA akaona ya kuwa maovu ya mwanadamu ni makubwa duniani na kwamba kila kusudi analowaza moyoni mwake ni baya tu siku zote. 8 Mwa 19:19;Kut 33:12;Lk 1:30;Mdo 7:46Lakini Nuhu akapata neema machoni pa BWANA.

    13 Eze 7:2;Amo 8:2;1 Pet 4:8Mungu akamwambia Nuhu, Mwisho wa kila kiumbe umefika mbele zangu; kwa sababu wameijaza dunia maovu, basi nitawaangamiza pamoja na dunia. 14 Jitengenezee safina ya mti wa mvinje; tengeneza vyumba ukaifunike kwa lami ndani na nje. 15 Hivi ndivyo utakavyoifanya; dhiraa mia tatu urefu wa safina, dhiraa hamsini upana wake, na dhiraa thelathini kwenda juu. 16 Uifanyie safina mwangaza, ukaumalize juu kiasi cha mkono mmoja; ukautie mlango wa safina katika ubavu wake; ukaifanyie dari tatu, ya chini, ya pili, na ya tatu.

  2. ONEN Versão Contemporânea Aberta em Suaíli

    5 Bwana akaona jinsi uovu wa mwanadamu ulivyokuwa mkubwa duniani, na ya kuwa kila mwelekeo wa mawazo ya moyo wake wakati wote ulikuwa mbaya tu. 8 Lakini Noa akapata kibali machoni pa Bwana.

    13 Kwa hiyo Mungu akamwambia Noa, "Nitawaangamiza watu wote, kwa kuwa dunia imejaa ukatili kwa sababu yao. Hakika mimi nitaangamiza watu pamoja na dunia. 14 Kwa hiyo jitengenezee safina kubwa kwa mbao za mvinje, tengeneza vyumba ndani yake na uipake lami ndani na nje. 15 Hivi ndivyo utakavyoitengeneza: Safina iwe na urefu wa dhiraa 300,6:15 Dhiraa 300 ni sawa na mita 135. upana wake dhiraa hamsini6:15 Dhiraa 50 ni sawa na mita 22:5. na kimo chake dhiraa thelathini.6:15 Dhiraa 30 ni sawa na mita 13:5. 16 Itengenezee paa na umalizie safina kwa kuacha nafasi ya dhiraa moja6:16 Dhiraa moja ni sawa na sentimita 45. juu. Weka mlango ubavuni mwa safina, na uifanye ya ghorofa ya chini, ya kati na ya juu.

Direitos das traduções citadas

Estes versículos te tocaram? Ore agora!

+581 estão orando agora.

Junte-se à corrente de oração.